Rooney Amechomoa Ofa Kibao za Umeneja.

Nyota wa Zamani wa machester United Wyne Rooney, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya DC United anasema kuwa amechomoa ofa kibao tu za kuchukua majukumu ya umeneja ili aweze kuzingatia kwenye majukumu yake kamamchezaji wa kulipwa kwa sasa.

Staa huyu anatarajia kuja kuwa mmoja wa mameneja bora zaidi watakaokuwa na mchango mkubwa katika soka baada ya kustaafu kama mchezaji wa kulipwa.

Rooney anakumbukwa vyema kwa historia yake ya magoli pale Manchester United na timu yake ya taifa ya Uingereza. Alipata mafanikio makubwa kwenye ligi ya Primia kabla ya kuamua kusepea DC united akitokea Everton mwaka 2018.

Mastaa wengi wa soka wa zamani wamekuwa wakiyanasa madili ya umeneja na kuendeleza kazi zao katika soka kwa njia nyingine tofauti na uchezaji baada ya kustaafu. Baadhi ya mastaa hawa ni kama Zienedine Zidane, Steven Gerrad, Frank Lampard, John Terry, na Scott Parker.

Wyne Rooney naye hayupo nyuma, licha ya kukiri kukataqa madili kibao ya umeneja, amesisitiza kuwa angependa kupambania fursa za umeneja baada ya kustafu soka.

“Ninachukua hatua kuhakikisha beji zangu (za ukocha) na nikimalizana na kucheza soka nitaangalia fursa ziatakazokuja mbeleni”

“Kuna ofa tayari nimeshapewa, lakini mbaka dakika hii mimi bado ni mchezaji na nahitaji kufurahia soka. Nitaangalia ofa zipi ni nzuri na kukamilisha.”

Acha ujumbe