Meneja wa Derby Country na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney anatajwa kuwa huenda akarithi mikoba ya Rafael Benitez ndani ya Goodison Park.
Everton siku ya Jumapili ilimfuta kazi aliyekuwa kocha wake Rafael Benetiz baada ya timu hiyo kuendelea kufanya vibaya ndani ya Premier League.
Ushindi wa Norwich City wa mabao 2-1 dhidi ya Everton ndiyo ulipelekea kibarua cha kocha huyo kuota nyasi, baada ya kocha huyo kudumu hapo kwa miezi sita tu. Akipoteza mechi 9 kati ya 12 za hivi karibuni.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuondolewa Benitez, Rooney ndiye ambaye kwa sasa anainoa Derby County ya Championship ndiye anatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kutua kwenye kikosi hicho.
Rooney ambaye aliwahi kuichezea Everton anapewa nafasi zaidi ya kwenda kukinoa kikosi hicho, japo kuna makocha wengine pia wanatajwa. Makocha kama Duncan Ferguson (msaidizi sasa) ambaye aliwahi kuishikilia kwa muda naye anatajwa kupewa timu, Frank Lampard na Jose Mourinho pia wamehusishwa.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA