Rooney Kurejea Uingereza

Ni nyota na mchezaji wa DC United amehudumu ndani ya soka kwa kipindi kirefu sana, Wayne Rooney ambaye alikuwa ni nyota aliyeng’ara sana na miamba wa soka Uingereza, United ambao wanatambua nafasi iliyochangiwa na uwepo wa mchezaji huyo kikosini kwao ambapo hakuwa na mafanikio kisoka pekee bali aliweza kuisaidia timu yake kuweza kunyanyua makombe ambayo kwa nafasi kubwa yameipa heshima United.

Lakini kadri historia inavyozidi kufunguka, mchezaji huyo bado amekuwa mwiba mbali na umri wake kusogea sana. Anasogea kwa awamu nyingine ndani ya jiji lililomlea na lililotambua uwezo wake katika klabu mpya mbali na ile ambayo aliweza kuichezea kwa kipindi cha nyuma akiwa kwenye kiwango chake.

Lakini kwa awamu hii anarejea akiwa kama kocha mchezaji ambaye anakwenda kujifunza zaidi baadhi ya mambo ambayo kwa upande wake anaangalia akiwa kama mchezaji anayetazamia kuwa kocha kwa siku za usoni ambako anaonekana ameweza kuwekeza nguvu zake kwa kiwango kikubwa. Jambo ambalo akiwa kama mchezaji mkongwe lina tija kubwa sana.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 kwa sasa anaangalia maisha nje ya kuwa uwanjani kama mchezaji ili aweze kupata maarifa mbalimbali kwa watangulizi wake ambao anategemea kujiunga nao ifikapo 2020 akiwa na malengo ya kubadili historia yake kutoka United akarudi zake Everton katika klabu ambayo ilimlea na kuweza kurejea kwenye ligi ya Marekani ambayo kwa historia huchukua wakongwe wengi sana.

Nyota huyo ameweza kunyanyua mataji 11 katika historia yake na kufunga zaidi ya mabao 359 katika ngazi ya klabu na taifa. Hatua ambayo kwa hakika ni kubwa sana na imeweza kumpa heshima ya aina yake akiwa kama mchezaji mwenye historia sana katika taifa hilo. Mbali na historia yake pia, amekuwa mchezaji wa Uingereza kuweza kukaa katika safari yake inayoridhisha sana kisoka.

Anatarajiwa kusaini kandarasi ya miezi 18 ikiwa na kipengele kinachomruhusu kuongeza kandarasi yake kwa kipindi kingine kama atakuwa tayari kufanya hivyo. Viongozi wa klabu hiyo akina Steve Kaplan wamejaribu kuliweka wazi kwamba nyota huyo anatimka klabuni hapo akiwa kama kocha mchezaji.

Japo bado ni swala la kujifunza na kuzidi kujiuliza kwamba kitu gani kimefelisha nyota huyo kurejea aidha kuchukua mbinu na maarifa kwa wakongwe walio ndani ya klabu ya Manchester au Everton ambako ameweza kulelewa kwa kipindi kirefu sana. Japo ujuzi unachukuliwa popote lakini alipaswa kupewa nafasi angalau ndani ya vilabu vyake ambavyo ameweza kuvihudumia kipindi chote.

2 Komentara

    Yuko sawa.

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe