Nyota wa zamani wa Manchester United, Wyne Rooney, amejitaja kuwa hakuwa mfungaji kwa asili lakini alikuwa na rekodi nzuri ya magoli Manchester United na Uingereza.

Rooney alichapa jumla ya magoli 253 na kuiondoa rekodi iliyokuwepo ya Sir Bobby Chalton pale United, wakati akiwa na rekodi ya magoli 53 kwa timu ya Uingereza kwa mechi 121 za kimataifa alizozicheza.

Rooney alihamia klabu ya MAnchester United mwaka 2004 na aliweza kucheza jumla ya mechi 559. Staa huyu anaamini kuwa alikuwa na nafasi ya kufunga magoli mengi zaidi lakini kwa bahati mbaya eyeye siyo mfungaji kwa asili! Bila shaka huyu anatania hapo!

Rooney alichapisha mengi kumuhusu kuhusu historia yake kwenye ukurasa wa Sunday Times, na kubainisha namna anavyojivunia kushikilia rekodi ya Man U na Uingereza.

“Ninashikilia rekodi ya magoli ya Manchester United na Uingereza na ninajivunia hilo, japokuwa wamekuwepo namba tisa ambao ni bora zaidi yake.”

Hata hivyo Rooney kwa nafasi yake amejitahidi kufanya vizuri katika kila timu ambayo namekuwepo na kuacha. Mpaka sasa yupo DC United toka mwezi Januari.

Rekodi ya Jumla ya Wayne Rooney
Timu Magoli Mechi
Everton (Aprili 2002-Agosti 2004) 17 77
Man Utd (Agosti 2004-Julai2017) 253 559
Everton (Julai 2017-Juni 2018) 11 40
DC United (Juni 2018-Januari 2020) 23 49
Derby County (Januari 2020-) 4 15
Uingereza (Februari 2003-Novemba 2018) 53 120

 

 

 

3 MAONI

  1. Hata hivyo Rooney kwa nafasi yake amejitahidi kufanya vizuri katika kila timu ambayo namekuwepo na kuacha historian kwa watu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa