Hispania: Aliyekuwa beki wa kati wa Chelsea na sasa Real Madrid Antony Rudiger amefunga bao lake la kwanza msimu huu akiwa katika timu hiyo hapo jana katika ushindi wa mabao 4-1 kwenye mchezo ambao walikuwa nyumbani kumkaribisha Mallorca.

 

Rudiger 29 Afunga Bao Madrid

 

Rudiger amejiunga na klabu hiyo msimu huu kutoka Chelsea ambapo ubora wake ulionekana sana wakati wa utawala wa Thomas Tuchel na hivyo kuvutia vilabu mbalimbali ikiwemo Juventus, Psg na Madrid lakini yeye akaamua kujiunga na mabingwa watetezi wa Laliga msimu uliopita.

Beki huyo wa Kijerumani  alifunga bao hilo la nne lililoiongezea Madrid mabao, lakini licha ya kujiunga na miamba hao wa Hispania bado hajawa chaguo pendwa kwa Carlo Ancelloti hivyo kupata nmba mara kwa mara inakuwa ni changamoto kwake hivyo anahitaji nguvu ya ziada na juhudi endapo akipata nafasi adimu kama hizo.

 

Rudiger 29 Afunga Bao Madrid

Rudiger na wenzake  mpaka sasa ndio vinara wa Laliga ambapo wameshinda mechi zao zote tano huku wapinzani wao wakuu Barcelpna wakiwafuatia kwenye nafasi ya pili huku tofauti yao ikiwa ni alama mbili kutokana na Barca kupata sare moja. Mechi inayofuata watawakaribisha RB Leipzig kwenye michuano ya klabu bingwa baada ya kupata ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Celtic.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa