Sadio Mane Kiungo mshambuliaji Raia wa Senegal anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundasliga, siku za hivi karibuni amekuwa akimfatilia kwa ukaribu mchezaji wa Simba ambaye ni Raia wa Senegal Pape Ousmane Sakho kutokana na kipaji alichonacho.

sadio mane, Sadio Mane Amtabiria Makubwa Sakho wa Simba, Meridianbet

Mane amejibu posti ya Sakho ambayo aliituma kupitia akaunti ya Twitter akionekana kumkubali mchezaji huyo wa Bayern na ndipo alipolazimika kuijibu kwa kuandika kuwa:

sadio mane, Sadio Mane Amtabiria Makubwa Sakho wa Simba, Meridianbet

“Asante sana kaka nakufuatilia pia, endelea kupambana na nina matumaini tutaonana timu ya taifa” Sadio Mane akimjibu Sakho.

Wawili hao ambao wote ni Raia wa Senegal walikutana nchini Morocco kwenye usiku wa tuzo za CAF kwa wachezaji wa Afrika wanaocheza nje na ndani ya Afrika, ambapo Sakho alifanikiwa kuchukua tuzo ya goli bora la mwaka, goli hilo aliwafunga Asec Mimosas kutoka nchini Ivory Coast kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika.

sadio mane, Sadio Mane Amtabiria Makubwa Sakho wa Simba, Meridianbet

Kwa upande wa Mane siku hiyo itabaki kuwa ya kihistoria kwenye maisha yake ya soka baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika akimpiku aliyekuwa mchezaji mwenzake wa klabu ya Liverpool Mohammed Salah ambaye ni raia wa Misri.

sadio mane, Sadio Mane Amtabiria Makubwa Sakho wa Simba, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa