Wakati matukio yote hayo yakija na mikakati ya kumwanga watu machozi. Mwaka 2003 Arsenal wao waliamua kupiga tukio la kuishtua dunia pasipo kuwahuzunisha watu. Walianza safari yao ya kucheza msimu mzima pasipo kupoteza mechi. Japo ilikuwa kama ndoto za Alinacha, walifika stand salama May 2004. Ligi ya timu 20, mechi 38 bila kupoteza hata moja.
Si Chelsea ya Claude Makelele na Frank Lampard, wala Liverpool ya Michael Owen na Steven Gerrard zilizopona. Walipigwa nje-ndani. Man United ya akina Ruud Van Nistelrooy walinusurika. Wakapewa sare mbili. Labda watoto wa juzi hawajui ile Arsenal, ngoja niwasimulie kidogo.
Alikuwepo mtu aitwaye Thierry Henry. Aliliona goli mara mbili zaidi ya binadamu wa kawaida, ni kama alikuwa ana macho manne. Mabao 30 msimu ule, nafasi ya pili kwenye ballon d’or. Ulitaka afanye nini cha ziada ili umkubali? Sitaki kumzungumzia mpishi Robert Pires na ile winga ya kushoto, sitaki kabisa kuyazungumzia mabao 14 aliyofunga ule msimu. Wala sitaki kumzungumzia muholanzi asiyepanda ndege, Denis Berkgamp.
Nataka kumzungumzia Adolf Hitler wa Ufaransa, Patrice Vierra. Mimi napenda kumuita ‘shetani wa dimba la chini’. Alibeba kila aina ya uchafu. Alikuwa na Arsenal wakati haina mpira, alipoupata aliikabidhi kwa “mchora ramani” Fred Ljunberg. Ljunberg akaifikisha Arsenal mbele.
Arsenal walikuwa na ukuta wa chuma wa Ashley Cole, Kolo Toure, Sol Campbell na Laureano Bissan. Waliruhusu mabao 26 tu msimu mzima. Ngome imara zaidi ya Chief Mkwawa wa wahehe pale Iringa.
Vile ndivyo Invicibles Arsenal ilivotokea. Baada ya Preston msimu wa 1888-89, haikuwahi kutokea invicibles nyingine ndani ya epl. Arsenal ndio waliirudisha.
mwakalosi
mwandishi embu tutake radhi man u sio walionusulika bali arsene Wenger alisema kuwa alijiona mwenye bahati kutokupoteza point zote kwa mzee Ferguson
Salma
Hakika ilikuwa istoria nzuri
Evaluziga
Ihistoria yake ili kuwa nzuri
Elika
Ilikuwa poa sana enzi hizooooo
Adelta
Anna history nzuri ktk maisha yake
Hukusu kucheza mpira
winfrida
kumbe arsenal waliacha historia nzuri inabidi wajitaidi tena kama walivyofanya 2004
Antony Luseno
Hii rekodi kuvunjwa tena pale EPL itakuwa ngumu sana
Hope mwaikuka
Enzi buana ilkua balaa
felister
natamani arsenal yangu ingerudi kwenye historia walioiacha ya mwaka 2003
Neema juma
Aiseee arsenal kumbe walifanya maajabuu matataaa.lazima wakumbukwe
Devotha
Asante sana leo umewatia moyo mashabiki wa arsenal
aisha
ni lazima wapate sifa kwa sababu Arsenal ni wapambanaji sana na wanajua umuhimu wa kuchapa kazi
Theckla
Ni historia ya kipekee sana na sijui km unaweza ikajirudia
Rehema
Ulikuwa safi sn kipindi hicho
Frank Patrick
Hakika hii historia kama liverpool ameikosa msimu huu hakuna wakuivunja …Unbeaten
Ernest
Ni Historia ambayo adi Leo wapenzi wa Arsenal wanatamba nayo kwenye vibanda umiza
Tahiya
Ni history ambayo haifutiki vichwani mwa mashabiki wa Arsenal
dorophina
Hii historia haitojirudia tena imeshapita
Hamidu
Wakati ule arsenal walikuwa na timu Bora
Maana mpaka muda huu record zao bado hazijavunjwa#meridianbettz
Ester jackson
Walikuwa wako vizuri sana ila hasaivi choka mbaya
Asia Abdy
History ya kipekee sana
David pere
Ilipendeza saana maana sisi mashabiki wake tulinenwpa ghafla bila kutarajia kwa burudani tuliokuwa tunaipata
Tatu
Arsenal ya zamani ilikuwa poa sana sio arsenal ya sasa awana maajabu
Amani
Arsenal walikuwa na ukuta wa chuma wa Ashley Cole, Kolo Toure, Sol Campbell na Laureano Bissan ilikuwa kiboko Sana hii #meridianbettz
Gabriel
Arsenal tuko vzur
Magdalena
Arsenal wapikuwa vizuri Sana
Furahav
Arsenal ya kipindi iko ilijaa na wachezaji vipaji na wanaojituma,ndomana walipata mafanikio sio wa sasa wote mabishoo tu.
Lombo
dah sidhan kama history itajirudia tena
Povel
Ni historian mpka leo haijafunjwa epl thnks meridian bet tz kwa update
Mwanahamisi
Ni historia ya kipekee sana
Kenani
Hii arsenal ndo ilinivutia mpk kufika moyon na kuishabikia
Emmy cleopa
Arsenal wako vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Ilikuwa bonge laistoria ilikuwa Atari sana mwendo wamchakamchaka ule
Swai
Alikuwepo mtu aitwaye Thierry Henry. Aliliona goli mara mbili zaidi ya binadamu wa kawaida, ni kama alikuwa ana macho manne. Alikuwa hatariii sana # meridianbet
Zeiyana
Arsenal ya zamani ilikua raha sana..!
Genia Sikaluzwe
Ni history nzuri ambayo haiwizi kuja kujirudia tena
Samiah
Arsenal ilikuwa nzuri sanaa zamani
Isaya massawe
Ilikua hatar sana
Sadick
Inafurahisha pale timu yako inaposhinda nje ndani. Arsenal inaweza kurejea zama zake#meridianbettz
Shafii
Ilikua arsenal ya aina yake iliyo kamilika kila sector
Mariam mtandama
Mzur