Kocha wa zamani wa Manchester United mwenye historia yake kwenye ligi kuu ya Uingereza aliwahi kusema kwamba, “kushambulia kunakufanya ushinde mechi yako, lakini kulinda kunakufanya ushinde mataji” akiwa na maana kwamba safu hizi mbili ni rafiki mno kwa klabu yoyote ile kuweza kushinda mataji na kupata ushindi kwenye mechi zinazochezwa.
Japo wengi wanaweza kuona kwamba usemi huu hauna uhalisia lakini ukweli ni kwamba katika klabu tano ambazo zinashiriki likgi kubwa tano duniani kuna klabu tatu kati ya tano ambazo zinasafu bora ya ulinzi na zinaongoza vizuri kwa kunyakua mataji, hivyo kauli hii ina ukweli mkubwa ndani yake kwa nafasi fulani. Ili kupata uhalisia zaidi, zifuatazo ni klabu zinazoongoza kwa kuwa na safu bora ya ulinzi:
Liverpool, kwa miaka mingi wamekuwa wakilega sana hasa upande wa safu hiyo ya ulinzi kwenye michezo yao mingi waliyoicheza. Lakini kwa sasa ni safu inayotisha kwa ulinzi kutokana na uwezo wao wanaouonesha. Usajili wao wa Virgil van Dijk kwa uhamisho uliovunja rekodi kwa hakika umeweza kuibua mengi kwenye safu hiyo ambao wamekuwa na mapatano mazuri na walinzi wengine. Hadi sasa katika mechi zao 35 wameweza kuruhusu magoli 20 pekee; hiyo ni kazi kubwa ya walinzi hao na mlinda mlango wao Alisson Becker.
Atletico Madrid, Diego Simeone anasifika sana kwa kazi yake kubwa ya kusuka safu ya ulinzi kwa miaka yote akiwa kama kocha wa klabu hiyo. Atletico wanasifika sana kwa kuwa na safu bora ambayo kwa hakika inahitaji nguvu na maarifa ya pekee kuweza kuipenya. Hadi sasa kwenye michezo 33 waliyoicheza wameweza kuruhusu magoli 21 pekee. Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba hawajaweza kuruhusu goli lolote kwenye mechi 19 walizocheza.
Manchester City, wakiwa chini ya Pep kwa hakika wamekuwa wakisifiwa kwa uwezo wao wa kushambulia japo hata eneo lao la ulinzi wapo vizuri kutokana na takwimu zinazowaonesha kwamba wanauwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi kutoka upande pinzani. Katika michezo yao 34 wameweza kuruhusu magoli 22 pekee ikiwa ni kiwango kizuri hasa kwa timu ambazo zina uwezo wa aina hii. Uwepo wa Aymeric Laporte umekuwa nguzo sana kwenye safu hiyo ambaye amekuwa akipambana kuweka sawa mazingira yote ya safu yao hiyo.
Juventus, kwa hakika ni klabu yenye safu imara ya ulinzi kwa kipindi kirefu sana. Wamekuwa na safu ambayo ni vigumu sana kuipenya na kuweza kuchukua alama kirahisi. Katika hatua hiyo wameweza kuruhusu magoli 23 kwenye mechi zao 33 walizozicheza; hiyo ikiwa ni uwezo wao waliouonesha kutokana na kuwa imara kuzuia maadui zao wasipate alama au ushindi mbele yao wa namna yoyote.
RB Leipzig, hawana nafasi kubwa sana katika ligi yao lakini sio wa kubeza wanapokuja katika takwimu za klabu yenye safu bora ya ulinzi. Wakiwa wameruhusu magoli 23 kwenye mechi zao 30 walizozicheza. Tangu Julian Nagelsmann achukue nafasi kama kocha kwa hakika ameweza kuijenga upya safu hiyo kwa heshima ya pekee sana.
Povel
Gud news