Saidi Ndemla Tayari Amehitimu Chuo Simba

Kama tungalikuwa kwenye karne ya 19 ningelichukua koti la mwanaharakati Martin Luther King na kumvisha Saidi mwana wa Ndemla.

Martin Luther king aliipigania haki za waafrika pamoja na kuendesha harakati za BACK TO AFRICA MOVEMENT. Tangu hapo akawa Engine na kiongozi wa watu weusi walionyanyaswa na kudharaulika kule Marekani.

Nimemshuhudia mtoto wa mzee Khamis akilitawala dimba la Mkapa kwenye usiku wa raha kwake. Nimeona mabadiliko makubwa sana kwake. Hapo awali nilishapoteza imani juu ya upigaji wake wa mashuti.

Nikasema kwenye kila mashuti 10 atakayopiga Saidi basi ni moja ndio litakua na madhara, sasa saidi amenidhihirishia hili. Amebadilika sana kwenye upigaji wa mashuti. Kwenye mashuti matano aliyopiga leo matatu yalikua na madhara.

Kadhalika Ndemla ameiprove kwenye pressing yake. Kipindi ambacho watu walimpigia kelele aondoke Simba ili akapate namba sehemu nyingne. Yeye akawaza kuwa yupo sehemu salama , akaigeuza Simba kuwa chuo cha soka kwake na sasa ameshagraduate. Huyo ndio Saidi bwanaaaa..

Ameimarika kwenye dribbling, accuracy na kuhold timu hata akiwa peke yake. Kuna mtihani anaupata Sven juu ya nani aanze na nani akae benchi kila anapoangalia viungo wake.

Pia leo nimemuona David Kameta DUCHU. Yupo vizuri ila krosi zake hazina madhara kabisa. Anahitaji kurudi kwa Kapombe na kupata somo la ziada juu ya upigaji wa krosi, krosi zake ziliishia kwenye ukuta wa mabeki wa maji maji.

Larry bwalya was on 🔥🔥. Ila nilifaidi sana kuiona pasi zake kuliko mikimbio yake. Hapa Tanzania kuna Luis Miquissone mmoja tu, Na leo amelithibitisha hilo.

Naamini Saidi Ndemla ni mwanaharakati aliyevumilia machungu ya benchi na leo anakua shujaa wa mchezo.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

20 Komentara

    Ndemla yuko zivuri sana namkubali

    Jibu

    Bado ngoja tuone uwezo wake kwenye mechi nyingine kwanza

    Jibu

    Ndemla jeshi

    Jibu

    Anajitahd

    Jibu

    Ni makin sana

    Jibu

    Tunasubiri tuone na mechi nyingine

    Jibu

    Yuko vizuli

    Jibu

    Ndemla anatisha

    Jibu

    Aongeze juhudi zaidi

    Jibu

    Ndemla yupo vizuri

    Jibu

    Jamaa anajua

    Jibu

    Dogo anajua huyo anamashuti ya mwendo kasi

    Jibu

    Ndemla yuko vizur

    Jibu

    Ni Makini sana

    Jibu

    Namkubalii

    Jibu

    Mambo mazuri hayatakagi haraka

    Jibu

    Ndemla yupo vizuri

    Jibu

    Jamaa Yuko poa

    Jibu

    JAmaa yupo vizur

    Jibu

    Ndemla ni mvumilivu sana

    Jibu

Acha ujumbe