Wakati Waholanzi kwenye Jiji la Rotterdam ndani ya dimba la Goffer wakishangilia kwa nguvu zote ili timu yao Feyenoord isawazishe dhidi ya NEC, ilikuwa bahati mbaya sana kwao hawakujua dakika chache zijazo nini kinakuja
Iliwekwa pass Moja ndefu sana kutoka kwa Golikipa wa NEC, ikaguswa na Midfielder mmoja kisha akaisukuma mali kwenye miguu ya Sniper mmoja wa hatari, katikati ya msitu wa mabeki

Akaicontrol ile mali, akaigusa touch ya kwanza kasi, akaigusa touch ya pili kwa akili, anatembea katikati ya mabeki wawili, akawatisha kulia na wakajaa kushoto, akamsalimia Golikipa kwenye nyavu za juu
Uwanja ukatulia kwa sekunde kadhaa, Saido Ntibazonkiza tayari anawakumbusha thamani ya miguu yake ya Kirundi, kila mtu alikubali, hii ilikuwa 2008 ligi kuu Uholanzi, alichofanya miaka 12 bado alikifanya jana kwa Kaseke
Uholanzi ilimuhusudu sana, lakini Mungu kaleta fumbo kubwa sana kwa watu wenye vipaji, kuna vitu katuficha kawapa maarifa, ujasiri na roho za kitajiri ila kuna namna kawafumba sehemu, fumbo la imaan
Saido nilimuona tena Ufaransa mechi kati ya Caen na Rennais, game tayari ngumu na dakika zinayoyoma na ushindi ni muhimu kwa Caen, kumbuka ni Ligi Kuu Ufaransa, Kocha anaagiza mipira yote ifikishwe miguuni mwake
Kaunta ya kwanza inafika kwa winga wa Caen, kisha ya pili inafika kwa straika wao, inawekwa kipa anaicheza, inawekwa ya pili beki anakataa, touch ya tatu inatua kwa Saido

Licha ya kuwa kwenye presha kubwa na nje kidogo ya 18, anaivuta mali, anachungulia wapi pakuweka na kumsabahi Golikipa, ngoma inaisha 1-0, Saido anaokoa siku kwa Caen
Hakuna jipya chini ya jua, Saido anaendeleza pale alipoishia, yaliyotokea yote ni fumbo la imaani, tuendelee kufaidi kipaji chake kinachoelekea mwishoni, Saido tulisafiri nyuma ya muda na sasa tupo mbele ya muda.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???




Shakila mrope
Anakipaji kizuri san tuenderee na kufaidi na kipaji chake
Issa
Mmh wape salaam saiid watamwez fund
Saupha mohamed
Jamaa yupo vizur
Rahmal
Jamaa namuelewa
Ernest Kimeru
Ngoja tuone
Adelta
Said ntibazonkiza ni mwenye kipaji Cha kuzaliwa
Lydia Emmanuel Magoti
Ngoja tuone
Hopemwaikuka
Amazing
warda
Ntibazonkiza anajua sana
Mwanahamisi
Ngoja tuone
Sarah
Yuko Safi tu
Tatu
Ngoja tuone