Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameweka wazi kua mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Mohamed Salah amerejea kwenye mazoezi ya pamoja na wenzake baada ya kusumbuliwa na majeraha aliyoyapata akiitumikia timu yake ya taifa.
Salah alipata majeraha wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Misri katika michuano ya mataifa ya Afrika ambayo yamemueka nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu, Lakini mchezaji huyo yuko mbioni kurejea dimbani na kuanza kuitumikia klabu hiyo.Klabu ya Liverpool ilikosa uwepo wa mshambuliaji huyo kwenye michezo kadhaa lakini sasa wana matumaini kua ataanza kuitumikia klabu hiyo, Kwani mchezaji akianza kufanya mazoezi na wenzake kuna asilimia kubwa za kuweza kurejea uwanjani kuitumikia timu.
Staa huyo wa kimataifa wa Misri amekua mhimili kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu ya Liverpool kwa takribani miaka saba sasa, Hivo taarifa za kurejea kwake uwanjani ni taarifa njema zaidi kwa mashabiki wa klabu hiyo pamoja na benchi la ufundi la timun hiyo likiongozwa na Jurgen Klopp.Mshambuliaji Mohamed Salah ni aina ya wachezaji ambao wana uwezo mkubwa wa kuamua mchezo, Hivo kurejea kwake kwenye timu ni wazi anaenda kuongeza nguvu kubwa kwenye kikosi cha Liverpool ambao wako kwenye mbio za ubingwa katika msimu huu wa mwaka 2023/2024.