Sami Khedira anaendelea kuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Juventus chini ya Andre Pirlo. Hii ni baada ya kusota kwenye benchi akiwa hajacheza mchezo wowote mpaka sasa.

Mkataba wa Khedira unamaliza mwishoni mwa msimu huu na uwezekano wake wa kuondoka kwenye Ligi ya Serie A ni mkubwa.

Everton na Tottenham ni miongoni mwa vilabu vya EPL vinavyoiwania saini ya Sami Khedira. Uwepo wa Carlo Ancelotti na Jose Mourinho ambao wote ni makocha waliowahi kufanyakazi na Khedira, unasemakana ndio kigezo kikubwa kinachompa nafasi mjerumani huyo kutua EPL.

Sami Khedira, Sami Khedira Anaitamani EPL., Meridianbet
Carlo Ancelotti akizungumza na Khedira walipokuwa Real Madrid.

Sami Khedira amenukuliwa akisema “kama itatokea fursa, nitaichagua Premier League (EPL). Mimi ni shabiki mkubwa wa Premier League Kumekuwa na maneno kuhusu kocha wa Everton – Carlo Ancelotti na kocha wa Tottenham – Jose Mourinho, hatujawahi kupotezana hata baada ya maisha ndani ya Real Madrid.

Licha ya kwamba huenda Sami Khedira ataondoka Juventus, mchezaji huyo amesisitiza hilo halitotokea kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Sami Khedira, Sami Khedira Anaitamani EPL., Meridianbet
Khedira akiwa na Jose Mourinho wakati wakiwa Real Madrid.

“Nitakapo ondoka, ninataka mashabiki wa Juventus wanikumbuke kama mchezaji mzuri. Hali iliyopo kwa sasa sio kwasababu ya Andre Pirlo, wala sinahasira kwa sababu hiyo. Ninaelewa namna anavyotaka kucheza mpira.

“Haitotokea mimi kuondoka Januari. Nitautumikia mkataba wangu mpaka majira ya joto 2021.” Alisema Khedira kupitia televisheni ya ZDF ya Ujerumani.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Sami Khedira, Sami Khedira Anaitamani EPL., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa