Sanamu ya Ibrahimovic Yatambulishwa Rasmi!

Sanamu ya aliyekuwa nyota wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic imetengenezwa kwenye mji aliozaliwa. Mashabiki wengi walijitokeza kushuhudia kutambulishwa rasmi kwa sanamu hiyo Jumanne.

Sanamu hii inatajwa kutengenezwa na msanii wa Uingereza, Peter Linde ina urefu wa futi 8 na inchi 9, na ina uzito wa karibia kilogramu 500.

Nyota huyu mwenye miaka 38 amefunga jumla ya magoli 62 kwenye mechi 116 za timu ya taifa ya Swiden kati ya mwaka 2001 na 2016.

Ibra alianza soka lake la kulipwa akiwa na Malmo kabla ya kwenda kujiunga na Ajax, kisha Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan, PSG na Manchester United. Mwaka 2018 alihamia nchili Marekani kucheza ligi ya MLS.

Anaungana na orodha ya mastaa wakubwa ambao wamepewa heshima kwa kutengenezewa sanamu wakiwemo David Beckham, Cristiano Ronaldo na Mo Salah.

 “Haijalishi unatokea wapi, upo wapi, haijalishi una muonekano upi, sanamu hii ni alama kuwa chochote kinawezekana” -Ibrahimovic.

Sanamu ya Ibrahimovic Yatambulishwa Rasmi!
Sanamu ya Zlatan Ibrahimovic

2 Komentara

    Safi

    Jibu

    Hiyo ni nembo ya ukumbusho na inabaki kuwa historia kwa mazuri aliyoyafanya kwenye game

    Jibu

Acha ujumbe