Sancho Aendelea kukiwasha Dortmund

Winga wa klabu ya Manchester United aliye kwa mkopo kwenye klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho ameendelea kua na mwendelezo mzuri wa kiwango ndani ya Borussia Dortmund.

Jadon Sancho amekua na kiwango kizuri tangu arejee Borussia Dortmund jambo ambalo limeibua hisia kubwa miongoni mwa mashabiki wa Man United wengine wakiona kama mchezaji huyo alionewa ndani ya United.sancho

 

 

Winga huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye aliondoka ndani ya Man United baada ya kugombana na kocha wake Erik Ten Hag, Huku yeye akiacha miguu yake iongee kwasasa ndani ya Borussia Dortmund.

Inaelezwa mabosi ndani ya klabu ya Man United wanafurahishwa na kiwango cha winga huyo, Kwani wanaamini akiendelea kuonesha ubora ndani ya Dortmund watapata kiwango kuzuri cha pesa wakihitaji kumuuza katika majira ya yajayo ya joto.sanchoKwasasa Jadon Sancho anafanya vizuri ndani ya Borussia Dortmund ambapo usiku wa jana alifanikiwa kuiwezesha klabu yake hiyo kutinga hatua ya robo fainali akifunga goli moja kwenye ushini wa mabao mawili walioupata dhidi ya PSV Eindhoven.

Acha ujumbe