Sancho Arejea Mazoezini United

Nyota wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho amerejea kwenye mazoezi ya klabu hiyo baada ya kukaa nje ya timu hiyo kwa takribani miezi kumi.

Winga Jadon Sancho ambaye alikaa nje ya klabu ya Man United tangu mwezi wa tisa mwaka jana baada ya kuingia kwenye mgogoro na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag, Ambapo baadae alitumia miezi sita akiwa klabu ya Borussia Dortmund kwa mkopo wa nusu msimu.sanchoTaarifa zinaeleza kua ndani ya wiki hii winga huyo alifanya mazungumzo ya ana kwa ana na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag na kufikia muafaka wa kumaliza tofauti zao, Jambo ambalo limemfanya winga huyo leo rasmi kurejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Jadon Sancho anatarajia kuwepo kwenye michezo ya kirafiki ya klabu hiyo ya kujiandaa na msimu mpya wa 2024/25 jambo ambalo linatoa taswira nzuri kwa mchezaji huyo na timu hiyo, Licha ya kua klabu hiyo imemueka sokoni mchezaji huyo lakini kuna uwezekano akasalia ndani ya timu hiyo kuelekea msimu ujao kutokana na kile ambacho atakionesha kwenye kipindi hiki cha kujiandaa na msimu mpya.

Acha ujumbe