Sancho Bado Yupo Sokoni

Winga wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho bado yupo sokoni kutokana na taarifa zinavyoeleza na klabu hiyo ipo tayari kumuachia kama watapata ofa nzuri kutoka kwa timu inayomuhitaji.

Klabu ya PSG ambayo ndio ilielezwa kua mstari wa mbele kuhitaji saini ya winga Sancho inaelezwa bado Man United haijapokea ofa yeyote kutoka kwa klabu ya PSG, Hivo mpaka sasa winga huyo anaweza kusalia ndani ya klabu hiyo kama hakuna ofa nzuri ambayo itawasilishwa mezani.sanchoSuala ambalo lipo wazi ni kua Manchester United wapo tayari kumuuza winga huyo wa zamani wa Borussia Dortmund lakini endapo tu watapata ofa nzuri, Mpaka sasa hakuna klabu ambayo imetuma ofa rasmi kumuhitaji winga huyo ambaye hajakua na wakati mzuri tangu ajiunge na timu hiyo.

Winga huyo licha ya kumaliza tofauti zake na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag lakini mustakabali wake ndani ya Manchester United, Huku mashetani wekundu wanachokihitaji kwasasa ni kupata kiwango cha pesa ambacho kitawasaidia kurahisisha sajili ambazo wanataka kuzifanya sokoni.sanchoKusalia kwa winga Jadon Sancho ndani ya Manchester United kutategemea na ofa ambazo zitakuja ndani ya timu hiyo zikiwa hazikidhi vya timu hiyo, Lakini pia maamuzi ya kocha Ten Hag na uongozi wa timu hiyo  kama utaamua kumbakiza winga huyo ndani ya timu hiyo kuelekea msimu ujao.

Acha ujumbe