Sancho Kuhusika Dili la Chiesa

Winga wa klabu ya Manchester United ambaye alikua anakipiga kwa mkopo kunako klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho ana uwezekano wa kutimikia klabu ya Juventus ya nchini Italia.

Inaelezwa winga huyo wa kimatiafa wa Uingereza anaweza kua sehemu ya dili la winga wa Juventus Federico Chiesa ambaye anahitajika na klabu ya Man United , Hivo Sancho anaweza kua sehemu ya mabadilishano hayo kuhakikisha dili hilo linakamilika.SanchoKlabu ya Juventus wameonesha nia ya kumtaka Sancho hivo Man United na wao wanaona ni nafasi ya kumchukua kiungo Chiesa ambaye amewekwa sokoni ndani ya klabu hiyo, Dili hili linaonekana halitakua gumu kwakua vilabu vyote viko tayari kuwaachia wachezaji wao.

Man Uited wameshatangaza kua wako tayari kumuuza Jadon Sancho halikadhalika upande wa klabu ya Juve upo tayari kumuuza winga wake Federico Chiesa, Sasa dili litakalopigwa hapa ni mabadilishano ya wachezaji hao lakini inaelezwa klabu ya Man United wao watahitaji na nyongeza ya pesa kidogo.

Acha ujumbe