
Winga huyo ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2021 kwa uhamisho paundi milioni 73 lakini klabu hiyo kwasasa imekubali kupata hasara ya pundi milioni 33, Kwani iko tayari kumuuza winga huyo dau la paundi milioni 40.
Winga Jadon Sancho atauzwa ndani ya Man United bila kujalisha kocha ambaye ataiongoza klabu hiyo kuelekea msimu ujao, Kama watafanikiwa kumuuza winga huyo wamepanga kumsajili winga wa Crystal Palace Michael Olise akiwa ndio yupo kwenye orodha ya juu kabisa ya wachezaji wanatakiwa klabuni hapo.