Kylian Mbappe ameamsha tena minong’ono juu ya hatma yake pale PSG. Hii ni kufuatia kauli yake aliyoitoa juu ya watu ambao anawachukulia kama mifano kwenye soka. Mpaka sasa Kylian Mbappe anahusishwa na klabu ya Real Madrid na Liverpool huku PSG wakijaribu kumuongezea mkataba kusalia klabuni hapo.
Mkataba wa sasa wa Mbappe na PSG unaisha mwaka 2022, hatma yake klabuni PSG imeendelea kuwa na sintofahamu huku ripoti zikitaja kuwa staa huyu haonekani kuwa na mpango wa kuongeza mkataba klabuni hapo.
Madrid wanatajwa kuwa wanapanga kufanya kila wawezalo kuinasa saini yake na wameamua staa huyu awe kipaumbele katika dirisha la uhamisho linalokuja.

Inakumbukwa kuwa Mbappe alishawahi kusema kuwa atakuwa wazi kusaini mkataba na Real Madrid katika siku zijazo. Lakini katika kuwataja wachezaji wake anaowakubali zaidi katika soka ameibua hisia tofauti baada ya kutaja kuwa meneja Zinedine Zidane, akifuatiwa na Cristiano Ronaldo ndiyo watu wanaomvutia zaidi na angependa kuacha nyayo kama zao.
Minong’ono inayoendelea sasa ni kuwa nani atakayeinasa saini yake? Je ni PSG wanaojitahidi kumshawishi kuongeza mkataba au ni Real Madrid ambako alikuwa anatamani kuwepo ili amfuate moja ya “Icon” wake katika soka, ama ni Liverpool ambao pia wamehusishwa naye kwa mda na wakijipanga kumleta kinda huyu wa miaka 21 kwenye Ligi ya Uingereza.

“Wa kwanza alikuwa ni Zidane, kwa kila kitu alichofanikiwa akiwa na timu ya taifa, na pia anakuja Ronaldo. Wote wameacha alama kubwa katika historia ya mchezo. Na ninataka kuacha kurasa zangu kwenye vitabu vya historia” -Mbappe
Kwa upande wa Liverpool, Klopp ambaye anapenda kumtaja Mbappe kama “Mashine” anatarajia kumnasa staa huyu hasa baada ya klabu hiyo kuhusishwa na kampuni ya Nike, ambao wanafikiriwa kuwa wanaweza kudhamini uhamisho wa staa huyu.
Hapa tunasema saini ya Mbappe sasa ni Sandakalawe! Mwenye kupata apate, huenda PSG wakafanikiwa kumbakiza au Liverpool wakafanikia kumshawishi au akamfuata Icon wake Zidane.


Antony Luseno
Bora aongeze mkataba na PSG
Carolyne
Yupo vizuri
Magdalena
Mbappe no mchezaji mahiri sana
#meridianbet
Hamidu
Talent player#meridianbettz
dorophina
Mbape mchezaji mzuri abaki tu PSG
Juliana
Mbappe mashine bwana
Povel
Mbappe haende Madrid#
Zeiyana iddi
Mbappe..!pasua miamba kijana
Ester jackson
Aongeze tu mkataba na PSG
Mwajuma
Bora aende madrid kwa zidane
David pere
Tatizo anauzwa Bei kubwa Sana wapunguze Bei kidogo
Evaluziga
Bora aongeze mkataba na PSG
Mariam mtandama
Yupo vizur
Samiah
Bora aende madrid kwa zidane
Neema hassan
Mbappe fundii..kikubwa aangalie maslah kwenye dau nono aende…
Elika
Mbape yupo vizur
Hope mwaikuka
Mbape namkubal sana
Aziza mushi
Mbappe aende Madrid tu
Theonestina
Mbape Yuko poa sana
Swai
Mbappe yuko vizuri aende kwa zidane
Agness
Yuko vizuri
Rehema Dickson
Mbappe yuko vizuri popote kambi
Mwanaidi
Yuko vzr sana mbape
Rehema
Mbape Yuko vzr sn
Emmy cleopa
Yuko vizuri
frank patrick
Nikiiona NIKE tu natia mtiki Anfield bhana
Hidaya Mohammed
Psg wakaze tu aendelee kubaki kwao
aisha
Mbappe anatisha namkubali sana
Adelta
Mbappe Ni jembe
mwakalosi
Mbappe atulize kichwa katika maamuzi
Neema juma
Jembee sana mbappe
Devotha
Abaki PSG
Warda
Kwa nini asiende Manchester #Meridianbettz
SADICK
Ningependa kumuona Mbappe akiwa Real Madrid#meridianbettz
winfrida
namkubali sana mbappe mchezaji mzuri sana
Latifa juma mohamed
Mbappe mchezaj Bora wa kombe la dunia,napendelea akienda liverpool
Kenani
Bora abaki psg
Amani
Bora aongeze mkataba na PSG
Ernest
Mbappe akikaza muda sio mrefu atafikia levo za wakina Messi, CR7 na Neymar
Gabriel
Habar njema
#meridianbettz
Mwanahamisi
Yupo vizuri
christopher
ABaki tu PSG, akuze kipaji zaidi
Shafii
Mbape yuko vizuri
Asha
Mbappe mchezaj mzuri sana
Samira
Mbape yupo vizuri sana angeelekea real madrid
Asia Abdy
Namkubal mbappe
Lombo
aende Madrid mpira pesa bhn
Salma
Mbappe mchezaji mzuri
Furahav
Mbape anajua sana.
Lydia Emmanuel Magoti
Mbappe kiungo mzuri jembe hilo
Ester mmakasa
Mbappe katika ubora wake ,namkubali sana.
felister
Mbappe haendi kokote