Mkuu wa uhamisho wa Sportitalia Alfredo Pedullà anadai Leicester City wamemtafuta Maurizio Sarri, lakini kocha huyo wa zamani wa Lazio anasubiri ofa bora zaidi.
Sarri aliamua kuondoka Lazio mwezi Machi na hana haraka kuchagua nafasi yake inayofuata. Tayari amehusishwa na majukumu ya kuinoa Fiorentina, Bologna na Panathinaikos.
Ndugu mteja usisahau kuwa meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Sasa Sportitalia wanaripoti kuwa Leicester City wamezungumza na kocha huyo, wakitumai anaweza kuchukua nafasi ya Enzo Maresca, ambaye amehamia Chelsea msimu huu wa joto.
The Foxes wana historia maarufu na makocha wa Italia, baada ya kushinda taji la Ligi Kuu na Claudio Ranieri. Sarri pia si mgeni katika soka la Uingereza, baada ya kushinda kombe la Ligi ya Europa akiwa Chelsea.
Leicester City ndio wamejihakikishia kupanda tena EPL, wakiwa kileleni kwenye msimamo wa Championship.
Huku wakiwa wamemtafuta kocha huyo wa zamani wa Napoli, Sportitalia wanabainisha kuwa hana nia ya kujiunga na Leicester City na anasubiri mapendekezo mengine ya kuvutia zaidi.