Golikipa wa zamani wa Manchester United na Manchester City Peter Schmeichel amesema kuwa Erling Haaland ana sifa nyingi za Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic ambapo amesema kuwa mshambuliaji huyo wa Manchester City ni sawa na washambuliaji kadhaa ndani ya mchezaji mmoja.
Mchezaji huyo alionyesha mchezo mzuri sana hapo jana wakati City ikiitandika Manchester United mabao 6-3 kwenye mchezo wa Dabi siku ya Jumapili, huku Haaland akifunga hat-trick yake ya tatu msimu huu, huku mchezaji mwenzake pia Phil Foden akifunga hat-trick yake ya kwanza.
Haaland ambaye ni raia Norway anafikisha mabao 14 katika mechi 8 za kwanza za Ligi kuu na hat-trick zote hizo amefunga katika uwanja wao wa nyumbani mfululizo na kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo katika historia ya mashindano hayo.
Kutokana na uwezo na ubora alionao Haaland wa kuizamisha United Schmeichel aligundua kufanana kati ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na hadithi kadhaa za kushangaza.
“Sehemu kubwa ya mshambuliaji mzuri ni uvumilivu. Nilicheza dhidi ya baadhi ya washambuliaji bora, na wanapokosekana ndipo unapolazimika kuelekeza nguvu,” mlinda mlango huyo wa zamani wa United na City aliambia BBC Radio 5 Live.
Schmeichel anaendelea kusema kuwa unapomtazama Haaland, unaona wachezaji tofauti, goli alilofunga ni kama Zlatan, na Ronaldo yumo pia unaona washambuliaji wa juu ndani ya mmoja. Ndio maana ni hatari.
Haaland na mchezaji mwenzake Kevin De Bruyne wamekuwa pea moja ambayo haishikiki huku De Bruyne akifukuzia rekodi mbalimbali za kuweka assist nyingi EPL, wakati huo huo ndio wanaonekana kuwa City ina mfungaji bora na mtoa assist bora msimu huu katika ligi tano bora.
Haaland tayari ameshazifumania nyavu mara 17 msimu huu, huku mabao matano kati ya hayo yakiwekwa wavuni na De Bruyne, ambaye ana jumla ya asisti 10 mnamo 2022-23.