Scotland iliilaza Ukraine 3-0 katika ligi ya Mataifa katika kipindi cha pili kutoka kwa John McGinn na mchezaji wa akiba Lyondon Dykes ambaye alifunga mabao mawili kwa vichwa na kufanya ubao usomeke tatu bila mpaka dakika za 90.
Baada ya kupoteza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa mpinzani sawa miezi mitatu iliyopita, vijana wa Steve Clarke walitawala mchezo huo wakati huu, ambapo mafanikio yalikuja katika dakika za 70 za mchezo ambapo McGinn alipoweka mpira kwenye kona ya chini baada ya kupokea pasi iliyomgusa mchezaji wao.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Scotand hao wako kileleni mwa kundi lao la ligi ya Mataifa, wakiwa pointi mbili mbele ya Ukraine huku kukiwa na mechi mbili za kucheza . Mfungaji wa mabao McGinn aligusia majira ya kukatisha tamaa kwa Scotland na jinsi alivyokuwa akicheza akiwa na uhakika wa kuthibitisha, Alisema kuwa;
“Tulichokuwa tukikosa wakati wa kiangazi ni kile tulichoonyesha Wembley, kile tulichoonyesha hapa dhidi ya Denmark: hasira, hamu, na sifa zote za timu ya Scotland ambazo tulikuwa nazo kwa namna fulani”.
“Kwahivyo ilikuwa muhimu kwamba tufanye upya na meneja aliweka wazi kuwa haikuwa nzuri vya kutosha. Tulikuwa tunacheza na point kuthibitisha usiku wa leo ambapo mlinzi mdogo wa Everton Nathan Patterson alilazimika kutoka uwanjani kwa machela wakati wa kipindi cha kwanza na Clarke akatoa taarifa yake kuhusu hali hiyo.