Senegal Yatinga Fainali AFCON 2021.

 

Timu ya Taifa, Senegal imefuzu katika fainali yao ya tatu ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2021 huku Sadio Mane akifunga na kuwasaidia kuwalaza 3-1 Burkina Faso.

 

Katika mechi iliojaa mbwembwe na bashasha , VAR ilikataa nafasi mbili za penati kwa upande wa Senegal , huku kipa wa Burkina Faso Herve Koffi akijeruhiwa katika tukio la kwanza .

Abdou Diallo na Idrissa Gueye waliipatia uongozi Senegal kabla ya Blati Toure alifunga goli la kufutia machozi dakika ya 82.

LMane alifunga goli la tatu na kuipatia timu yake ushindi mkubwa. Lilikuwa goli la 29 la Mane kwa taifa lake , na kumuweka sawa na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Henry Camara.

Senegal sasa itakabiliana na Misri au waandaji wa michuano Cameroon katika fainali itakayopigwa siku ya siku ya Jumapili.

Burkina Faso nayo itashiriki katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo ambayo itachezwa siku moja kabla ya fainali hiyo.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe