Timu ya taifa ya Serbia inaonekana bado inachechemea kwenye michuano ya Euro 2024 baada ya kuambulia alama moja kwenye michezo miwili ya makundi ambayo wamecheza mpaka sasa.
Serbia ambao leo wamecheza mchezo wao wapili kwenye michuano ya Euro leo dhidi ya Slovenia wamepata sare baada ya kusawazisha goli dakika za jioni sana kabisa, Kwani walikua tayari wameshatanguliwa kwa goli moja kwa bila na timu ya taifa ya Slovenia.Mchezo wa leo ulianza kwa kasi ambapo Serbia walionekana kutengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini wakashindwa kuzitumia na kupelekea mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya bila kufungana, Lakini kipindi cha pili kilikua cha Slovenia ambapo walifanikiwa kupata goli dakika ya 69 kupitia Ž. Karničnik.
Serbia walionekana kuhaha kusawazisha bao hilo baada ya kushindwa kutumia nafasi nyingi walizozitengeneza kipindi cha kwanza, Katika kuhakikisha wanapata goli la kusawazisha walianza kufanya mashambulizi makali langoni mwa Slovenia ambao wao pia walikaa nyuma baada ya kupata goli dakika ya 95 Luca Jovic akafanikiwa kuwasawazishia bao ambalo lilifanya mchezo huo kumalzika kwa sare ya goli kwa moja.Mpaka sasa kundi B lipo wazi kwani Serbia wana alama moja wakati huo Slovenia wana alama mbili wakiwa wameshacheza michezo miwili, Huku wakisubiri mchezo wa Uingereza dhidi ya Denmark ambapo Denmark ana alama moja akifanikiwa kushinda au kufungwa bado inaendelea kutoa nafasi kwa Slovenia na Serbia katika michezo yao ya mwisho ya kukamilisha makundi.