Rasmi, Sergio Aguero atangaza kustaafu soka kwa sababu za kiafya. Hii ni baada ya kuitumikia Barcelona kwa miezi 6 tu.

Aguero alijiunga na Barcelona baada ya kumaliza mkataba wake na Manchester City mwishoni mwa msimu uliopita. Akiwa Barcelona, Sergio Aguero ameitumikia timu hiyo kwenye michezo 5 pekee kutokana na kupata majeraha ya mara kwa mara.

Sergio Aguero, Sergio Aguero Astaafu Soka., Meridianbet
Akiwa Man City, Aguero aliisaidia klabu hiyo kutwaa mataji 5 ya EPL na kupachika jumla ya magoli 184.

Oktoba 30, 2021, wakati akiwa uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Alaves [mchezo uliisha kwa matokeo ya 1-1], Aguero alitolewa uwanjani dakika ya 30 baada ya kupata tatizo la kifua na toka hapo, mchezaji huyo hajarejea tena uwanjani.

Kwa kuzingatia afya yake, Aguero ameamua kutundika daluga akiwa amecheza jumla ya michezo 786 na kupachika magoli 427.


ANZA MSIMU WA SIKUKUU NA BURST THE BANK

Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa