Sergio Aguero Yuko Tayari Kurejea Dimbani!

Sergio Aguero yuko tayari kurejea kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City kwa mara ya kwanza tangia Mechi ya Kombe la FA dhidi ya Birmingham.

Nyota huyu mwenye rekodi nzuri ya ufungaji rekodi nzuri ya magoli pale Manchester City, amecheza jumla ya mechi tisa tu msimu huu kwa sababu ya changamoto za kiafanya.

Staa huyu mwenye miaka 32 aliikosa sehemu ya mwisho ya msimu uliopita kwa sababu ya jeraha la goti kisha akafanyiwa upasuaji, na tatizo hilo pia limekuwa sababu ya yeye kukosa sehemu kubwa ya msimu huu mpya kwa hatua hii ambayo imefikia.

Sergio Aguero Yuko Tayari Kurejea Dimbani!

Meneja Pep Guardiola pia amekuwa akisuasua sana kufanya maamuzi ya kumuanzisha staa huyu kwenye mechi, akihofia karata anayoeweza kuicheza inaweza kuwa na matokeo gani. Hata hivyo, kwa sasa anaamini staa huyu anaweza kuwa tayari kurejea dimbani.

Katika taarifa ya Guardiola, Aguero amekuwa na maendeleo mazuri na kwa siku 10 zilizopita ameonekana kuboreka zaidi mazoezini.

“Ataanza na kwa dakika ambazo hali yake na uwezo wake vitaruhusu. Kama anaweza kucheza dakika 90 itakuwa safi, au 60 au 30 itakuwa sawa. Kitu muhimu ni kuhakikisha anakuwa na mda wa kutosha kadri iwezekanavyo na kuona hali itakuwaje.” -Maneno ya Pep Guardiola wakati wanajiandaa kushuka dimbani dhidi ya Birmingham City Jumapili.


 

JIUNGE NA FAMILIA YA MERIDIANBET BURE!!!!

Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??

BOFYA HAPA

15 Komentara

    Imekaa powa sana

    Jibu

    Mungu amtie nguvu aendelee kupachika magoli

    Jibu

    Safi sana arguero

    Jibu

    Karibu Sana mambo yanazidi kunoga

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Habari njema hizi

    Jibu

    Arejee tu itapendeza sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Namashaka na fitness ya Aguero kutokana na majeruhi yake ya mara kwa Mara

    Jibu

    Vizuli sana arguero

    Jibu

    Nmeipenda hii

    Jibu

    Safiii

    Jibu

    Kun iz back

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Itakuwa poa sana

    Jibu

Acha ujumbe