Serie A na Corona

Wachezaji watatu wa Fiorentina na wafanyakazi watatu wa Klabu hiyo wamepimwa na kukutwa na virusi vya Corona. Vilabu vya Serie A vimepewa ruhusa na serikali ya Italia kuendelea tena na mazoezi, ingawa wachezaji wanaweza kufanya mazoezi peke yao.

Wachezaji na wafanyakazi hao wametengwa na kundi lote litakuwa na vipimo vya matibabu na utimamu.

Pia Mchezaji mmoja Torino na wachezaji wanne wa Sampdoria wote walipima na kukutwa na virusi vya ugonjwa huo na kuwekwa kwenye kizuizi.

Wachezaji wa Sampdoria

Lakini hakuna klabu ambayo imetaja majina ya wachezaji ambao wamekutwa na COVID 19 kwani hufanywa siri, ili kupunguza mfadhaiko kwa jamii.

Italia imeanza kupunguza vizuizi vyake baada ya kufungwa kwa wiki nane. Vilabu vya Serie A vimerudi kwenye mazoezi lakini hakuna uamuzi juu ya lini Ligi kama itaanza tena. Wachezaji wote watafanyiwa vipimo kwanza ndipo waendelee na mazoezi binafsi.

4 Komentara

    Tahadhari ni muhimu kuchuliwa ili kuepusha mlipuko mkubwa wa wagonjwa kwa wachezaji.

    Jibu

    umakini unahitajika sana maana kwa hali kama hiyo hakuna usalama kabisa kwa wachezaji

    Jibu

    afya n jambo la kuzingatiwa sana

    Jibu

    Duuh poleni sana ndugu zangu

    Jibu

Acha ujumbe