Mambo yanakuwa matamu Serie A, viwanjani ni mchaka mchaka. Leo Torino wanajianda kuwatumia vyema Andrea Belotti na Simeone Zaza dhidi ya Parma, wakati Cagliari wakisafiri bila kuwa na nyota wao Radja Nainggolan

Serie A: Torino vs Parma

Torino akivaana na Parma wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa baada ya kupoteza mechi saba mfululizo. Wanatarajiwa wanaweza kutumia 4-4-2 wakiwatanguliza Belotti na Zaza. Kwa upande wa Parma, watakuwa wanaingia dimbani wakiwa na Dejan Kulusevski wa Juventus aliyepo hapo kwa mkopo.

Serie A: Verona vs Cagliari

Cagliari wakiwa chini ya kocha mpya, Walter Zenga kwa mara ya kwanza wanaingia dimbani bila kuwa na Nainggolan ambaye anasumbuliwa na jeraha. Zenga hatarajiwi kufanya mabadiliko makubwa zaidi ya 4-3-1-2 kama mtangulizi wake.

Vikosi Vinavyotarajiwa

Torino vs Parma

Torino: Sirigu; De Silvestri, Izzo, Nkoulou, Djidji; Edera, Rincon, Meite, Berenguer; Belotti, Zaza

Parma: Sepe; Darmian, Iacoponi, Bruno Alves, Gagliolo; Kucka, Hernani, Kurtic; Kulusevski, Cornelius, Gervinho

Verona vs Cagliari

Verona: Silvestri; Rrahmani, Kumbulla, Gunter; Faraoni, Amrabat, Veloso, Lazovic; Pessina, Zaccagni; Borini

Cagliari: Cragno; Cacciatore, Ceppitelli, Pisacane, Pellegrini; Nandez, Cigarini, Rog; Birsa; Pereiro, Simeone

49 MAONI

  1. Leo mechi zote kal ila kwa upande wa cagliar tunatarajia kuona maajabu kupitia kwa Walter zenga maana inavyoonekana ndo mechi yake ya Kwanza tokea alivyoingia club hiyo n mtanange wa nguvu sana na mfumo wake nao uko vzur sana ila inaasikitisha kuona kuwa nanggolon hatokuwepo lakin tunasubiri maajabu ya mfumo wa 4_3_1_2 kutoka kwa zenga

  2. Hizi mechi kazi kazi hakuna lele mama maana watu wamekaa kwa muda mrefu na timu zote zinataka kukaa mahali pazur wakisaka point

  3. Mechi zaleo zipo vizuli apo sisi wateja kujipangilia tuu leo tuchezeje mikeka yetu kwasababu mechi nzuri Odds zakibabe patamu hapo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa