Klabu ya Aston Villa imemteua Craig Shakespeare kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo akichukua nafasi ya John Terry.

John Terry alikuwa msaidizi wa Dean Smith katika kukinoa kikosi cha Aston Villa kilichopambana kubaki Ligi Kuu Uingereza- EPL. Aston Villa ambayo ilipanda daraja msimu uliopita, walikuwa na wakati mgumu kupambana kusalia kunako EPL msimu ujao.

Dean Smith na John Terry
Dean Smith na John Terry

Terry amekuwa akipewa lawama za mara kwa mara kwa kushindwa kutumia uzoefu wake kama beki hodari kuboresha safu ya ulinzi ya Aston Villa. Pamoja na changamoto zote, Terry kwa kushirikiana na Dean Smith walifanikiwa kuibakiza Villa kwenye Ligi Kuu Uingereza – EPL baada ya Watford kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Arsenal.

Shakespeare anauzoefu mkubwa na EPL akiwa amewahi kufanya kazi na Claudio Ranieri kukinoa kikosi cha Leicester City. Katika wakati wake na Leicester City, walifanikiwa kubeba kombe la Ligi Kuu Uingereza – EPL mwaka 2015/16.

Shakespeare
Shakespeare akiwa na wachezaji wa Leicester City

Craig Shakespeare Akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Leicester City.

Taarifa rasmi kutoka katika ukurasa wa Aston Villa zinasema ” Nilikuwa ninahitaji kuongeza mkufunzi mahiri wa Ligi Kuu Uingereza – EPL katika benchi langu la ufundi, Craig anakila sifa katika hilo.”

” [Shakespeare] anauzoefu mkubwa, atatuongezea viwango vingine katika timu yetu. Nimemfaham Craig kwa muda mrefu, tangu kipindi tunacheza Walsall. Ninatarajia mazuri katika kufanya nae kazi” Alisema kocha mkuu wa Aston VillaDean Smith.

Craig amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika Ligi Kuu Uingereza – EPL na ligi daraja la kwanza – Championship.

Akiwa na miaka 56 [Craig Shakespeare], amewahi kuwa kocha msaidizi na pia, amewahi kuwa kocha mkuu. Kwa ujumla amekuwa kwenye benchi la ufundi kwa takribani miaka 20 akishiriki michezo 500.


Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.

Ingia Mchezoni

34 MAONI

  1. Terry licha ya kua mzoefu tu katika safu ya ulinzi kwa upande mwengine ilipaswa avumiliwe kwani bado ni kinda Sana katika sector ya ukocha na anasafari ndefu ya kuja kua kocha mzoefu.

  2. Unaweza kuwa mwanafunzi mzuri lakini usiwe mwalimu mzuri. Terry bado hajakomaa kuwa kocha mwenye mafanikio,anahitaji muda. Aston Villa imeona mapungufu na kuamua kubadili mwelekeo#meridianbettz

  3. Bado sana kwa kocha mana katika uchezaji wake alikuwa vizuri ila bado hajastahili kuwa kocha sio kitu cha wepesi

  4. Terry angeenda tuu kua mchambuz kuliko hyo kali anayo ifanya au basi akaunge nguvu na frank lampard kwenye kikos cha Chelsea kama marejendari wawili waliochezea club moja

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa