Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Luke Shaw amekubali kutokua chaguo la kwanza klabuni hapo chni ya kocha Eric Ten Hag.

Beki huyo hakua na malalmiko baada ya kuachwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo toka mwezi wa nane na kukubali kuna kitu mwalimu huyo anataka kubadilisha kwenye timu hiyo.

shawShaw ambaye alianza michezo miwili ya awali katika timu hiyo dhidi ya Brighton, na Brentford na kupoteza michezo yote miwili na kua mara ya kwanza kwa timu hiyo kupoteza mechi mbili za mwanzo wa msimu kwa miaka 30.

Baada ya hapo mchezaji huyo hajatokea kwenye kikosi cha kwanza tena kwenye michezo minne ya mbele ambayo klabu hiyo imeshinda.

Luke anaamini atacheza kwenye timu hiyo mara kwa mara kabla ya michuano ya kombe la dunia nchini Qatar na hata kutokupangwa na kutokana na Tyrell Malacia sio kitu kilichomshangaza.

Alipoulizwa kuhusu kucheza kombe la dunia nchini Qatar “Nafikiri kila mtu ndo anachotaka. “Nadhani Ten Hag anajua sifa zangu,anajua ninachoweza kufanya na tumekua kwenye mazungumzo

shaw“Inaeleweka kabisa mwanzo wa msimu haukua mzuri,Na ilihitajika afanye mabadiliko hilo hata mimi nalikubali kabisa” Kitu pekee nachoweza kufanya ni kufanya mazpezi kwa bidii, Na kusubiri nafasi yangu kwenye kombe au michezo ya ligi kuu”

“Chochote ninachocheza, lazima niwe tayari kucheza kwenye kiwango kinachohitajika“Alizungumza hayo baada ya mchezo waliotoka suluhu ya magoli matatu kwa matatu dhidi ya Ujerumani usiku wa jana.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa