Kibwana Shomari Tumika, Maana Yanga Walituma na Yakutolea

Mshairi mkongwe Abdallah Kizere aliwahi kunena kuwa👇”Fikiri zako fikira, ufikiri kila tendo, Fikiri lilo na dhara, ufikiri na Ia pendo.  Fikiri lililo tohara, ufikiri na uvundo, “kisha akasema shairi hili liitwe FIKIRI. Ni kweli kibwana shomari AMEFIKIRI.
.
Njozi zinanirudisha 1993 mitaa ya Jangwani walipoketi manguli wa Yanga wakijipongeza kwa kazi kubwa, Namzungumzia Zamoyoni Mogela, Abubakar Sure boy, Saidi Mwamba Kizota na winga mbunifu Edibily Lunyamila. Kikao hiki kilimuhusu beki wa kulia Mwanamtwa Kihwelo.

Zamoyoni Mogela wakwanza kushoto

Haikua ajizi juu yao, bali ni pongezi kwa kazi nzuri ya kuutawala mrengo wa kulia pale Jangwani. Mwaka huo Yanga walichukua ubingwa wakiwa na mechi 5 mkononi. Chini ya mwalimu wa kirundi marehemu Nzoisaba Taurany huyu aliisaidia yanga kutwaa taji la club bingwa Afrika Mashariki.
.
Huenda Cedric kaze akairudia historia ya mrundi mwenzie kunako Jangwani kwa kumpika sawiya beki Kibwana Shomari. Anyways.. leo Tanzania inashuhudia maamuzi ya kiume yanayofanywa na mvulana Shomari Kibwana. Ameamua kuipambania namba kwenye timu ya taifa, amekunywa sumu ya ukomavu.

Kibwana Shomari akiwa Mtibwa

Kibwana huyu sio yule wa Mtibwa, kule alikua na joho na sasa anavaa gwanda la kivita kila akiingia kazini. Accuracy yake imeongezeka, intensity yake imepanda, kasi yake imechachamaa. Huyo ndio Shomari bwana. Leo hii anaifanya kazi ya Shedrak Nsajingwa na Juma Abdul kwa wakati mmoja. Ile morali ya MWANAMTWA imehamia miguuni kwa Kibwana.

Juma Abdul

Anajua jinsi ya kutuma na ya kutolea kwa mastriker wake. Hivi sasa Tuisila haangaiki tena, anasubiria mali kutoka kwa kibwana kisha aitupie kati. Leo hii tumemsahau Paul Godfrey, hatumkumbuki tena Juma Abdul. Shomari amekua sasa, ametoka utotoni na ameamua kufanya kazi za kiume.

Uthubutu na nia thabit ndio sitiari za Kibwana. Natambika kwa mizimu ya Jangwani, nakemea mapepo ya kasi na kusi, mashariki na magharibi nachoma ubani juu ya milima ya Uruguru kumpongeza mwanaume aliyejitoa kwaajili ya yanga, Yes ni Kibwana Shomari. Kila la kheri kwake, upande wa kulia upo salama sasa. Si Yanga tu bali hata timu ya taifa letu tulivu. Shomari is now matured.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

13 Komentara

    Hapo zamani yanga walikuwa na kikosi kizuri sana

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Wakipambana wataweza

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Shomari kazi kwako mashabiki tunataka Kuona mafanikio makubwa kwa sababu wametuma nayakutolea

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Kaz kwake

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Tunataka tuone majabu kazi kwake

    Jibu

    Mguu adimu

    Jibu

    Yupo kawaida sana

    Jibu

    Kazi kwake

    Jibu

Acha ujumbe