Majira ya Jioni ya tarehe 17 Agosti 2017, Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Younes Abouyaaqoub mwenye umri wa miaka 22, aliendesha gari kwenye barabara ya watembea kwa miguu eneo La Rambla huko Barcelona ​​​​Hispania, na kuua watu 13 na kuwajeruhi wengine 130, mmoja wao alikufa siku 10 baadaye tarehe 27 Agosti.

Baada ya kufanya tukio hilo Abouyaaqoub alikimbia na kisha akamuua mtu mwingine ili kuiba gari lake atoroke. Saa tisa baada ya shambulio la Barcelona, ​​wanaume watano wanaodhaniwa kuwa wanachama wa genge moja la kigaidi waliingia kwenye eneo la Cambrils, na kuua mwanamke mmoja na kuwajeruhi wengine sita. Wote watano wa washambuliaji hao walipigwa risasi na kuuawa na polisi.

Barcelona, Siku Isiyosahaulika kwa Barcelona na Wapenzi wa Soka kote Duniani, Meridianbet

 

Usiku wa kabla ya shambulio la Barcelona, ​​mlipuko ulitokea katika nyumba moja katika mji wa Uhispania wa Alcanar, na kuharibu jengo hilo na kuwaua washiriki wawili wa kundi la kigaidi, akiwemo imamu mwenye umri wa miaka 40 anayefikiriwa kuwa ndiye alikuwa mchora ramani.

 

Nyumba hiyo ilikuwa na zaidi ya mitungi 120 ya gesi ambayo ndani yake polisi wanaamini kuwa kulikuwa na utengenezwaji wa bomu moja kubwa au ‘mabomu matatu madogo zaidi ili wayaweke kwenye magari matatu waliyokuwa wameyakodisha’ lakini waliyalipua kwa bahati mbaya.

Barcelona, Siku Isiyosahaulika kwa Barcelona na Wapenzi wa Soka kote Duniani, Meridianbet

Waziri Mkuu wa Hispania wa wakati huo Mariano Rajoy, alitaja shambulio la Barcelona kuwa shambulio la kijihadi. Shirika la Habari la Amaq lilihusisha uwajibikaji usio wa moja kwa moja wa shambulio hilo kwa Islamic State.

Mashambulizi hayo yalikuwa mabaya zaidi nchini Hispania, tangu mashambulio ya bomu ya treni ya Machi 2004 huko Madrid, na mabaya zaidi kutokea Barcelona tangu shambulio la Hipercor la 1987. Mtuhumiwa Younes Abouyaaqoub ​​aliuawa na polisi huko Subirats, mji ulioko kilomita 31 (maili 19) magharibi mwa Barcelona tarehe 21 Agosti.

Polisi nchini humo waliwakamata wanaume wanne kuhusiana na mashambulizi hayo, watatu walikamatwa huko Ripoll ambao ni mmiliki wa gari lililotumiwa katika shambulio la Cambrils, kaka wa Moussa Oukabir, na mtu wa tatu ni Mohamed Houli Chemlal mwenye umri wa miaka 20, ambaye alinusurika kwenye mlipuko wa Alcanar pia alikamatwa.

Washukiwa wa Uharifu

 

Mohamed Houli Chemlal na Driss Oukabir walishtakiwa kwa uanachama wa shirika la kigaidi, na mauaji huku Mohamed pia akishtakiwa kwa kupatikana na vilipuzi. Wote wawili walipatikana na hatia, ingawa waliachiliwa kwa mashtaka ya mauaji ya kigaidi.

Kufikia tarehe 24 Agosti 2017, wawili kati ya washukiwa, Salh El Karib na Mohamed Aalla, walikuwa wameachiliwa kwa masharti maalum, ikiwa ni pamoja na kuzidhibiti hati zao za kusafiria.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa