Silva Apanga Kucheza Soka Hadi Miaka 40s

Beki wa kati wa Chelsea, Thiago Silva ambaye leo hii ni siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 38 amesema kuwa anapanga kumuiga rafiki yake Zlatan Ibrahimovic kucheza soka hadi atakapotimiza miaka 40 na kuendelea.

 

Silva Apanga Kucheza Soka Hadi Miaka 40s

Silva, 38 leo, amekuwa mmoja wa wachezaji waliocheza vizuri zaidi Chelsea wakati ambao umekuwa mwanzo wa msimu kwa misukosuko. Ana nia thabiti ya kuiongoza Brazil kwenye Kombe la Dunia msimu huu wa baridi na amedhamiria kupanua uchezaji wake mzuri kwa muda mrefu iwezekanavyo.

Beki huyo mkongwe wa kati amekuwa akipokea vidokezo kutoka kwa mchezaji mwenzake wa zamani wa AC Milan na  Psg Ibrahimovic ambaye atafikisha miaka 41 mwezi ujao. Thiago alisema; “Ninazungumza mara kwa mara na Zlatan na hivi karibuni mara nyingi zaidi kwasababu Chelsea itacheza dhidi ya AC Milan Ligi ya Mabingwa.

 

Silva Apanga Kucheza Soka Hadi Miaka 40s

“Lengo langu ni kucheza hadi nifikishe miaka 40 lakini sijui kama itakuwa kwa kiwango hiki au mashindano haya. “Inategemea msimu huu na tutaona kitakachotokea Katika Kombe la Dunia. Inategemea pia kuongezwa kwa mkataba. Lakini ndio lengo langu ni kucheza hadi niwe na umri wa miaka 40”

Mkataba wa sasa wa Silva huko Stamford Bridge unamalizika mwishoni mwa msimu. Lakini nahodha huyo wa Brazil haonyeshi dalili ya kupungua kasi kwa klabu au nchi na Bosi mpya wa Blues Graham Potter huenda atamtegemea pakubwa kama Frank Lampard na Thomas Tuchel walivyofanya.

Gwiji wa Chelsea Lampard alikuwa kocha wakati Silva anajiunga na Chelsea kama mchezaji huru mnamo Agosti 2020 baada ya kuachana na PSG. Aliendelea kuwa mchezaji wa kawaida chini ya Tuchel, ambaye pia alisimamia beki huyo wa kiwango cha juu katika mji mkuu wa Ufaransa, baada ya kuteuliwa kwake London Magharibi mnamo Januari 2021.

 

Silva Apanga Kucheza Soka Hadi Miaka 40s

Potter alimuanzisha Silva katika mchezo wake wa kwanza akiwa kama kocha mpya wa Chelsea katika mchezo wa ligi ya Mabingwa kwenye mchezo ambao walitoka kwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya RB Salzburg.

Acha ujumbe