Simba Anakufa kwa Mkapa - Kaze

Cecrick Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa licha ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kupelekwa mbele wanaamini kwamba wakikutana ndani ya uwanja lazima washinde.

Awali ratiba ilikuwa inaeleza kuwa mchezo huo wa watani wa jadi ulitarajiwa kuchezwa Februari 20, Uwanja wa Mkapa ila kwa sasa utachezwa Mei 8.

Kaze alisema kuwa hawana mamlaka ya kuzungumzia kuhusu kubadilishwa kwa ratiba ya mchezo ila wanachojua wao ni kwamba lazima watakutana ndani ya uwanja.

“Kubadilishwa kwa ratiba hiyo kwetu sio tatizo, kwa kuwa mamlaka imesema iwe hivyo sisi tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo ambapo kwa sasa tupo kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbeya City.

 

“Kwa kuwa tutakutana nao Mei 8 hiyo basi tunajipanga kuona kwamba tukikutana nao uwanjani tunashinda. Kwetu tunatazama mechi zote ni ngumu na ushindani ni mkubwa hivyo hatuna mashaka lazima tufanye vizuri,” alisema.

Mchezo wa raundi ya kwanza walipokutana uwanjani, Yanga ikiwa mwenyeji ngoma ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Mkapa.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

12 Komentara

    Maneno mengi hatutaki ngoja tuone

    Jibu

    Izo ni mbwembwe tu ngoja tuone itakuwaje

    Jibu

    Sisi mashabiki tunasubiri kwa hamu hiyo mei8

    Jibu

    Maneno yasiwe mengi sana ni vitendo siku hiyo

    Jibu

    Mmh

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

    Ataanzaje kufa kwamfano wazee wakazi

    Jibu

    Paka FC hawana jipyaa

    Jibu

    Mechi ya Yanga na Simba haijawahi kuwa rahisi hata kama timu mojawapo haina kikosi mahiri

    Jibu

    Simba sio timu ya kuibeza

    Jibu

    Asije kufa yeye tu

    Jibu

Acha ujumbe