Nyota watatu wa Simba SC wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Mei (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao waliongia kwenye kinyang’anyiro hicho ni Bernard Morrison, John Boko na Taddeo Lwanga ambao mmoja wao atashinda kutokana na idadi ya kura atakazopata.

 

Wachezaji watano waliingia kwenye kinyang’anyiro hicho lakini Kamati maalumu iliwachuja na kubaki na watatu ambao watapigiwa kura na mashabiki kupitia Tovuti rasmi ya klabu.

Tuzo hii ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile itakuwa ni ya nne kutolewa tangu ilipoanza mwezi Februari mwaka huu.

Mchezaji atakayepata kura nyingi atakabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium kushirikiana.

Miquissone alikuwa mchezaji wa kwanza wa Simba SC kutwaa tuzo hiyo mwezi Februari wakati Joash Onyango alishinda mwezi Machi na Cloutus Chama mwezi April.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa