Klabu ya Simba SC imeweka wazi bonasi zitakazotolewa kwa wachezaji ambapo wakishinda dau linakuwa kubwa, wakitoka sare dau linashuka na wakipoteza mechi hawapati chochote.

Mechi wanazoshinda ugenini ama nyumbani huwa wanalipwa kati ya Sh200 milioni na Sh230 milioni wakati sare inakuwa kati ya Sh100 milioni na Sh150 milioni.

Mechi ya ugenini dhidi ya Plateau United Simba walishinda bao 1-0, wachezaji walivuta Sh230 milioni wakati mechi ya marudiano nyumbani iliyoisha kwa sare walitoa Sh150 milioni.

 

simba, Simba Bonasi Kama Zote Kuelekea Fainali., Meridianbet

“Katika mechi ya kwanza dhidi ya Platinum ya Zimbabwe wachezaji hawakuvuta kitu kwa sababu walifungwa bao 1-0, lakini mechi ya marudiano Benjamin Mkapa walishinda mabao 4-1, wachezaji walivuta Sh200 milioni.

“Hatua ya makundi tulianza kwa ushindi wa bao 1-0, ugenini dhidi ya AS Vita wachezaji walipata Sh200 milioni, mechi ya pili tulishinda bao 1-0, dhidi ya Al Ahly nyumbani walichukua Sh230 milioni,” alisema na kuongezea;

“Mechi ya tatu tulitoka sare ugenini na Al Merrikh ya Sudan ambapo walipewa Sh200 milioni, marudiano tulishinda bao 3-0, wakachukua tena Sh230 milioni.”

Mjumbe huyo wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC anasema baada ya hapo walicheza mechi ya tano hatua ya makundi na AS Vita na kushinda bao 4-1 bonasi yake ilikuwa ni Sh230 milioni.

Alisema walipokwenda kukamilisha ratiba hatua ya makundi ugenini dhidi ya Al Ahly walifungwa bao 1-0, hapo hawakupata bonasi yoyote.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

simba, Simba Bonasi Kama Zote Kuelekea Fainali., Meridianbet

CHEZA HAPA

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa