Mabingwa watetezi wa VPL, Simba wameondoka Dar leo Ijumaa, kuelekea wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi watakapocheza mechi ya kiporo dhidi ya wenyeji wao Namungo ambao wametoka kushinda bao 1-0 mchezo uliopita dhidi ya Gwambina.
Mechi hiyo itachezwa Jumamosi katika Uwanja wa Majaliwa huku wenyeji Namungo wakihitaji ushindi ili kumaliza katika timu za juu kama ilivyo kwa Simba ambao wanasaka ushindi ili kurahisisha kazi katika mbio zao za ubingwa.
Kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema lengo la kwanza lilikuwa kucheza nusu fainali Ligi ya mabingwa Afrika lakini limeshindikana hilo na wamebakiwa na malengo mawili makubwa.
Alisema lengo la kwanza kwao wanataka kuchukua ubingwa wa kombe la shirikisho (ASFC), pamoja na ligi kuu ambao utawapa nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Lazima kiwake