BAADA ya kufika Misri na kuanza mazoezi, timu ya Simba inatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki kwa ajili ya kujiweka fiti.

Baadhi ya wachezaji walioweka kambi Misri tayari wameanza mazoezi jana katika mji wa Ismailia.

 

simba, Simba Kucheza Mechi Tatu Misri., Meridianbet

Akizungumzia kambi yao, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa “Tunashukuru Mungu tulifika salama na kikosi kilianza mazoezi rasmi jana na leo pia waliendelea.

“Wachezaji wa awamu ya pili wanatarajia kufika kesho wakiongozwa na Moses Phiri na Nassoro Kapama ili kujiunga na wengine kwa maandalizi ya ligi.”

Kikosi cha hicho kimetimkia Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu pamoja na michuano ya Klabu bingwa Afrika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa