Simba Kutafuta Tiketi Hatua ya Makundi

Klabu ya Simba leo inashuka dimbani majira ya saa kumi kamili jioni kumenyana na klabu ya Ahly Tripoli katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwajili ya kutafuta tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Wekundu wa Msimbazi leo watahitaji kupata matokeo ya ushindi wa aina yeyote ili kufuzu hatua ya makundi kwani mchezo wa kwanza ambao ulipigwa nchini Libya ulimalizika kwa sare ya bila kufunga, Hivo namna pekee klabu hiyo inaweza kufuzu hatua ya makundi ni kushinda mchezo wao wa leo wakiwa nyumbani.simbaKlabu ya Ahly Tripoli inacheza na Simba katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa tahadhari kubwa kwakua inatambua ubora ambao timu hiyo imekua nao pale wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, Lakini hiyo haitowazuia kuhitaji ushindi kwani kwa upande wao pia wanahitaji ushindi au sare ya mabao ili kufuzu hatua inayofuata.

Mchezo wa leo ukimalizika kwa sare ya magoli ina maana Ahly Tripoli watakwenda hatua ya makundi ya kombe la shiirikisho kutokana na sheria ya goli la ugenini ambayo bado inatumika kwenye michuano ya CAF, Hivo wekundu wa Msimbazi Simba wanapaswa kupata matokeo ya ushindi kwa namna yeyote ili wafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Acha ujumbe