Simba SC : Mashabiki 35,000 Waruhusiwa Shirikisho.

 

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 35,000 kuhudhuria mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Jumapili saa 10 jioni, Februari 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

CAF imetaka kufuatwa taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa corona kama kukaa kwa nafasi baina ya mtu na mtu, kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji safi.

CAF imesisitiza taratibu hizo kufuatwa hivyo kila shabiki anapaswa kuchukua hatua na kumlinda mwenzake aliye karibu yake kwa muda wote wa mchezo.

Uongozi wa klabu ya Simba SC umepanga kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika na taratibu zote zinafuatwa huku ukiwataka mashabiki kununua tiketi mapema muda ukifika ili kuondoa usumbufu siku ya mchezo.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe