Hii ni mara ya pili kwa Simba kukwamia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa katila misimu mitatu iliyopita kwani msimu wa 2018-2019 ilitolewa na TP Mazembe ya DR Congo kwa jumla ya mabao 4-1. Ililazimishwa suluhu nyumbani na kwenda kupasuka ugenini jijini Lubumbashi kwa mabao 4-1.
Pamoja na kutolewa katika michuano ya kimataifa, licha ya ushindi wa mabao 3-0 iliyopata mbele ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Simba imeendeleza rekodi yake ya nyumbani kwa leo kutimiza jumla ya miezi 99 bila kupoteza ikiwa jijini Da es Salaam.
Simba ilipata ushindi huo kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2020-2021, lakini imetoka kwa ushindi wa mabao 4-0 iliyopata Kaizer ikiwa kwao na kufanya itinge nusu fainali kwa jumla ya mabao 4-3.
Hata hivyo, licha ya kutolewa Simba imeendeleza rekodi katika michuano hiyo, ikiwa uwanja wake wa nyumbani katika michuano ya kimataifa kwani leo imetimiza jumla ya miezi 99 bila kupoteza katika ardhi yao.
Miezi hiyo ni sawa na siku 3016 au miaka nane na miezi mitatu na siku tano, tangu ilipopoteza mechi yao ya mwisho nyumbani dhidi ya Recreativo do Libolo ya Angola.
Simba ilicharazwa bao 1-0 na Waangola katika mechi ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa Februari 17, 2013 kabla ya kwenda kulala 4-0 ugenini waliporudiana Machi 3.
Mabao ya Simba katika mechi ya jana yalifungwa na nahodha John Bocco aliyetupia mawili na jingine likizamishwa kimiani na kiungo Mzambia Clatous Chama. Kaizer sasa wanaungana na watetezi Al Ahly ya Misri iliyolazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo ilikubali kichapo cha 2-0 kwenye mechi yao ya kwanza.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Safi