Kikosi cha Simba SC kimefanikiwa kupata alama moja ugenini dhidi ya US Gendarmerie Nationale ya Niger katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi uliopigwa Uwanja wa Jenerali Senyi Kountche nchini Niger.

 

simba sc, Simba SC Yaibuka na Alama Moja Shirikisho., Meridianbet

Wenyeji Gendarmerie walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12 lililofungwa na Gbeuli Wilfred baada ya kiungo Sadio Kanoute kufanya makosa katika eneo la hatari.

Kipindi cha pili Simba SC walirudi kwa kasi na kulifikia zaidi lango la Gendarmerie huku wenyeji wakicheza nyuma na kutumia mipira mirefu.

Mlinzi Pascal Wawa ambaye aliingia dakika ya 45 kuchukua nafasi ya Joash Onyango alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kutolewa nafasi yake ikachukuliwa na Kennedy Juma.

Bernard Morrison aliisawazishia Simba SC bao kwa kichwa dakika ya 83 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Shomari Kapombe.

Sare ya leo inawafanya Simba SC kufikisha pointi nne baada ya mechi mbili na kuongoza kundi D.

Msimamo wa kundi D ulivyo:

• Simba SC 🇹🇿 = 4 points
• ASEC Mimosas 🇨🇮 = 3 points
• RS Berkane 🇲🇦 = 3 points
• USGN 🇳🇪 = 1 point


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa ndege yako na ujishindie zawadi kibao.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa