Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji Moses Phiri raia wa Zambia aliyekuwa anachezea Zanaco FC ya nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili.
Phiri ambaye pia anaweza kucheza nafasi za kiungo mshambuliaji na winga zote mbili atavaa jezi nyekundu na nyeupe kuanzia msimu ujao wa mashindano.
Phiri ni usajili wa kwanza ndani ya Simba SC wanaolekea kwenye maboresho makubwa ya kikosi ambayo wamepanga kuyafanya kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuanza mapema hivi karibuni.
Msimu uliopita akiwa na Zanaco Phiri amefunga mabao 14 kwenye ligi kuu ya Zambia akiwa ni mfungaji bora namba mbili nyuma ya kinara mwenye mabao 16.
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.