Simba SC Yamuaga Rasmi Rally Bwalya.

 

Klabu ya Simba SC imethibitisha kumuuza kiungo mshambuliaji, Rally Bwalya leo Ijumaa jioni (Juni 16), baada ya kufikiwa kwa makubaliano rasmi kati ya pande hizo mbili.

Simba SC kupitia Simba APP imethibitisha taarifa hizo kwa kuwafahamisha mashabiki na wanachama wake, ambao katika kipindi hiki wamekua karibu na vyanzo vya habari vya klabu hiyo, ili kufahamu nani anasajiliwa na nani anaondoka klabuni hapo.

 

Taarifa ya Simba SC imeeleza: “Uongozi wa klabu yetu umefikia makubaliano ya kumuuza kiungo mshambuliaji Rally Bwalya kwa timu ambayo hatutaiweka wazi kwa sasa, kutokana na matakwa ya kimkataba.”

Bwalya alisajiliwa msimu wa 2020/21 akitokea Pawer Dynamo ya nchini kwao Zambia ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwezi huu, huku tetesi zikieleza kuwa huenda akajiunga na klabu ya Amazulu ya Afrika Kusini.

Akiwa msimbazi kiungo huyo alikuwa sehemu ya kikosi ambacho kilitwaa mataji yote na kuisaidia klabu hiyo kutinga robo fainali ya mashindano ya Afrika mara mbili mfululizo.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

Acha ujumbe