Klabu ya Simba SC imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation CUP (ASFC) kwa kishindo baada ya kuigalagaza Ruvu Shooting kwa magoli 7-0.

 

simba sc, Simba SC Yatinga Robo Fainali ya ASFC kwa Kishindo., Meridianbet

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa, mida ya saa moja usiku ulishuhudia kiungo wa Simba SC, Cloutus Chota Chama akiondoka na mpira baada ya kufunga magoli matatu ‘hatrick’.

Nahodha wa Simba SC, John Bocco alifunga bao la mapema dakika ya kwanza kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kiufundi na Yusuf Mhilu.

Chama alifunga bao la pili dakika ya 25 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Peter Banda kabla ya dakika mbili baadaye kufunga bao la tatu akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Mzamiru Yassin.

Bocco alitufungia bao la nne dakika ya 40 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Gadiel Michael kabla ya Michael Masinda alijifunga bao la tano katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Gadiel.

Kipindi cha pili Jimmyson Mwinuke alifunga bao la sita dakika 70 dakika chache baada ya kuingia baada ya kupokea pasi kutoka kwa Chama, kabla ya kiungo huyo kukamilisha karamu ya magoli na kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Israel Patrick.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa