UONGOZI wa Simba umempa kibarua kizito Kocha Mkuu, Zoran Maki cha kukagua wachezaji ambao wanafaa kuendelea na wale wa kuachwa kwenye timu kwa msimu huu.

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi ya msimu ujao kwenye mji wa Ismailia nchini Misri.

 

simba, Simba Wampa Kibarua Kizito Kocha., Meridianbet

Akizungumzia hilo, Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez, amesema kuwa “Kocha ana siku nyingi za kuangalia timu na atatushauri mchezaji gani ambaye anafaa kuendelea au hafai.

“Ni lazima tutumie fursa ya pre season (maandalizi) kwa ajili ya kuangalia hadhi za wachezaji wetu nani anastahili kuwepo na nani hastahili.

“Tunampa nafasi kocha ya kukagua kwahiyo kuanzia wiki ijayo hadi mwisho wa mwezi tutajua yupi anatoka kwenye timu, Kocha atakapotoa maoni basi tutayachukua na kutekeleza.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa