Simba Wasisitiza Hawajamaliza Kushusha Vyuma

Uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa mchakato wa usajili wa kikosi chao kuelekea msimu mpya wa 2026/27 bado haujafungwa, huku ukiwataka mashabiki kukaa tayari kwa utambulisho wa nyota wengine wapya hivi karibuni.

Simba Wasisitiza Hawajamaliza Kushusha Vyuma

Akizungumzia mipango ya klabu hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ameeleza kuwa kwa sasa viongozi wapo kwenye maandalizi ya mwisho ya safari ya kuelekea nchini Rwanda kushiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup, ambayo itatumika kama sehemu ya maandalizi (pre-season) ya kikosi hicho.

Ahmed Ally amebainisha kuwa ingawa tayari wamewatambulisha baadhi ya wachezaji waliopendekezwa na benchi la ufundi, bado wapo kwenye mazungumzo na nyota wengine.

Simba Wasisitiza Hawajamaliza Kushusha Vyuma

Usajili wetu bado haujakamilika. Leo tuliamua kupumzika kidogo ili kutoa nafasi kwa matangazo yaliyopita kueleweka vizuri, lakini kuanzia kesho tutaendelea na utambulisho wa wachezaji wengine wapya,” amesema Ahmed Ally.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kuhusu taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuondoka kwa wachezaji kama Libasse Gueye, Anicet Oura, Inno Loemba, na Selemani Mwalimu, Ahmed amezikanusha vikali taarifa hizo na kusisitiza kuwa nyota hao bado ni wachezaji halali wa Simba SC.

Amesisitiza kuwa Simba haitafanya maamuzi yoyote kwa kuongozwa na shinikizo la mitandaoni, bali itafanya maamuzi kwa maslahi ya klabu na kutoa taarifa rasmi kwa wakati sahihi.

Simba Wasisitiza Hawajamaliza Kushusha Vyuma

Katika hatua nyingine, Ahmed Ally ametangaza kuwa tamasha la Simba Day 2026 litafanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Hatua hii imekuja kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kuendelea kufanyiwa matengenezo.

Tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani litaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo kongwe nchini, huku mashabiki wakipata fursa ya kushuhudia kikosi kamili kitakachopeperusha bendera ya Simba SC msimu wa 2026/27.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.