SIMBA YAFAFANUA KWANINI WALIMPOTEZEA AZIZ KI

WAKATI wa dirisha la usajili mkubwa ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2024/25 zilivuma tetesi kwamba Simba ipo kwenye hesabu kubwa za kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki raia wa Burkina Faso.

Ikumbukwe kwamba kabla ya Ki kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga alikuwa anatajwa pia kuwa kwenye mpango wa kutakiwa na Simba zama hizo alipokuwa akikipiga ndani ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.SIMBAMwisho Aziz Ki aliongeza mkataba wa kuitumikia timu yake ya Yanga ambayo yupo mpaka sasa na walitwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2023/24 hivyo ni mabingwa watetezi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa walikuwa na mpango wa kuinasa saini ya Ki ila waliamua kumuacha kutokana na kuwa na jicho la mbali.

“Aziz Ki mkataba wake uliisha na tulikuwa na uwezo wa kumchukua Aziz Ki lakini tukafanya tathmini ya kiwango chake, tafsri yake ni kwamba kama angekuwa ndani ya Simba angekuwa anafanya kama yale ambayo alifanya Uwanja wa Azam Complex.

“Hakuna Mwanasimba ambaye angekubali kuona anafanya yale hivyo tuliamua kuachana naye kwa kuwa tulijua ambayo yangetokea, tukimtaka mchezaji sisi hatushindwi.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.