Simba Yamvutia Kasi Frederic Nsabiyumva

Bila shilingi milioni 958 za Kitanzania, Simba haiwezi kumpata beki wa kimataifa wa Burundi anayekipiga nchini Afrika Kusini katika Klabu ya Chipa United, Frederic Nsabiyumva.

Simba imekuwa ikimfuatilia mchezaji huyo kuanzia dirisha lililopita la usajili lakini iligonga mwamba kutokana na thamani yake.

Uongozi wa Simba baada ya kupewa ruhusa ya kuongeza wachezaji 10 kwa ajili ya michuano ya kimataifa msimu huu, ina mpango wa kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu mabao katika michezo ya ligi kuu jambo ambalo limewafanya kumrudia beki huyo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 25, anakumbukwa kwa kumkaba vizuri mshambuliaji Mbwana Samatta katika mchezo wa kirafi ki uliofanyika Uwanja wa Mkapa kati ya Tanzania na Burundi na Burundi kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Oktoba 11, mwaka huu.

Kuhusiana na thamani yake, wakala wa wachezaji katika Ligi ya Afrika Kusini anayejulikana kwa jina la Herve Tra Bi, aliliambia Spoti Xtra kuwa ili Simba waweze kumpata beki huyo, lazima walipe si chini ya euro 350,000 ambazo kwa Tanzania ni zaidi ya shilingi milioni 958.

“Simba wanatakiwa watoe si chini ya euro 350,000, hiyo inatokana na thamani aliyonayo mchezaji huyo na ubora wake bila kusahau umri na ligi anayocheza. Hivyo kama Simba watakuwa tayari kuilipia hiyo nadhani watampata.

“Ukiangalia Chipa United walimnunua kwa euro 225,000 (zaidi ya Sh milioni 616 za Kitanzania) kutoka Jomo Cosmos, hivyo lazima wamuuze kwa faida,” alisema wakala huyo.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

20 Komentara

    simba wakiweka mambo sawa wanaweza wakamchukua uyu jamaa

    Jibu

    Asanten kwa taarifa.

    Jibu

    Simba wakijipanga vizuri wanaweza kumchukua

    Jibu

    Simba mmeanza Mambo yenu

    Jibu

    Simba hawawez kumchukua huy mtu

    Jibu

    Simba nawakubali akuna linalo shindikana kwao wakimtaka mtu awanaga utata wakutoa pesa kwailo watuwatasubili Sana

    Jibu

    Simba lazima wamchukue

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Jamaa angechukuliwa na Simba ingekuwa poa

    Jibu

    Duu dau kubwa sana hilo sijui kama watafanikiwa

    Jibu

    Simba watamchukua tuu

    Jibu

    Hela zote hzo jamani

    Jibu

    Simba wakiamua wanaweza

    Jibu

    Dau kubwa sizan Kama Simba wanawez kufikiah dau hlo la mchezaj huyo ila ngoj tuone bodi ya usajil wa Simba imejipa ngaje ilikukamilisha dili hlo msimu huu

    Jibu

    Simba wako vizuri wanaweza

    Jibu

    Asante sana

    Jibu

    Shukrani kwa tahalifa

    Jibu

    Simba lazima wamchukue

    Jibu

    Asante sana

    Jibu

    Simba hawashidwi kitu

    Jibu

Acha ujumbe