Klabu ya Simba imerejea Dar es salaam kimya kimya majira ya usiku baada ya kushindwa kuvuna pointi tatu kwenye Ligi hapo jana walipokuwa wakimenyana na Mbeya City majira ya saa 10:00 jioni.

 

Simba Yarejea Dar Kimya Kimya

Simba walikuwa ugenini hapo jana kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya ambapo walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 baada ya kutangulia kupata bao kupitia kwa kiungo wao Mzamiru na baadae bao hilo kusawazishwa na Tariq Seif.

Mchezo ulikuwa wakufunguka kwa kila timu huku Simba wakihitaji pointi tatu kupunguza gepu lililopo kati yao na vinara wa ligi Yanga ambao hawajapoteza mchezo wowote kwenye ligi hadi sasa.

Baada ya sare hiyo Wekundu wa Msimbazi wanasalia nafasi ya 3 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 13 wakiwa na pointi 28 wakiwa wameachwa pointi moja na Azam ambaye ana pointi 29.

Simba Yarejea Dar Kimya Kimya

Vilevile Mbeya City wao baada ya sare ya hapo jana wapo nafasi ya 6 na pointi zao 19 kibindoni huku mchezo unaofuata wakitarajia kumenyana na mabingwa watetezi Yanga siku ya Jumamosi.

Wakati Simba wao watasafiri kukipiga dhidi ya Polisi Tanzania ambao bado wana hali mbaya kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 13 wakiwa na pointi 9 nafasi ya 14.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Simba, Simba Yarejea Dar Kimya Kimya, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa